
Macron aikosoa Marekani kujiondoa mkataba wa Iran
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amesema maamuzi ya rais Donald Trump wa Marekani ya kujiondoa kwenye mkataba wa nyuklia wa Iran yalikuwa ni makosa.
Macron alipozungumza na vyombo viwili vya habari vya Ujerumani vya DW na ARD wakati wa ziara yake humu nchini hapo jana kwamba mkataba huo unahitaji kile alichosema kuwa ni “kumaliziwa” lakini akisisitiza kwamba ni njia bora zaidi ya kuidhibiti Iran na shughuli zake za kinyuklia zenye lengo la kujilinda.
Amesema, amesikitishwa na maamuzi hayo na anahisi kuwa hayakuwa sawa. Awali, Macron alizungumza na rais wa Iran Hassan Rouhani na kumuelezea nia ya Ufaransa ya kuuendeleza mkataba huo.
Macron alimweleza Rouhani azma hiyo kwenye mazungumzo kwa njia ya simu huku akisisitiza umuhimu wa Iran pia kufanya hivyo. Kwa pamoja viongozi hao wamekubaliana kuendeleza ushirikiano pamoja na mataifa mengine yanayohusika.