
Madereva wa vyombo vya moto nchini watashurutishwa endapo watavunja…
Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani nchini, kamishna msaidizi mwandamizi, FORTENATUS MUSILIMU amesema hayo wakati akizungumza na maderevya hao katika kituo cha MABASI cha zamani na kipya mkoani TABORA.
Amewataka madereva wote kutimiza vigezo vya usafiri kwanza ndipo wapeleke vyombo vyao barabarani, kinyume na hivyo watakamatwa na kufungiwa leseni zao.
Baadhi ya madereva wamempongeza kamanda MUSILIMU kwa mikakati yake ambapo pamoja na mambo mengine wameeleza uhusiano wao na Askari wa usalama barabarani mkoani TABORA kuwa sio mzuri.
Aidha kamanda MUSILIMU ameendesha zoezi la kukagua abiria katika mabasi na kupima madereva kama wanatumia kilevi katika kituo kipya cha mabasi.
Dereva aliyepimwa na kubainika hatumii kilevi anayeendesha gari kutoka USINGE hadi BARIADI OMARI KASIMU, amesema ili kutowachukia Askari wa usalama barabarani ni vema madereva kufuata sheria kama zilivyo.
Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani nchini,kamishna msaidizi mwandamizi, FORTENATUS MUSILIMU yupo katika ziara mkoani TABORA kukagua hali ya usalama barabarani na kuzungumza na madereva wa vyombo vya moto pamoja na abiria lengo ni kupunguza na kumaliza ajali barabarani.