Mahakama ya rufaa TANZANIA Mkoani Tabora imeanza kikao cha…
Mahakama ya Rufaa TANZANIA imeanza kikao cha wiki mbili mkoani TABORA chini ya uenyekiti wa Jaji MBAROUK SALIM ambapo jumla ya mashauri 25 yatasikilizwa na kutolewa maamuzi.
Kwa mujibu wa Kaimu Msajili wa Mahakama ya Rufaa TANZANIA,AMIR HAMIS MSUMI,majaji wengine ni Jaji STELLA MUGASHA na Jaji JACOBS MWAMBEGELE.
Amesema kuwa kati ya mashauri yanayosikilizwa,Tisa ni ya rufaa za jinai,Sita ni maombi ya rufaa za jinai,matano ni rufaa za madai huku maombi ya rufaa za madai yakiwa ni matano.
Kaimu Msajili huyo amebainisha kuwa katika rufaa zinazosikilizwa na majaji hao ni zile za muda mrefu mpya zenye maombi ya dharura.