Skip to content
CGFM
  • Home
  • Listen Live
  • News
  • Presenters
  • Gallery
  • Advertise

Maisha ya pacha waliozaliwa wameshikana hatarini Gaza

  • October 24, 2017
Watoto hao walizaliwa Jumamosi na mmoja wao anatajwa kuwa dhaifu kuliko mwingine.

Maisha ya watoto pacha waliozaliwa wakiwa wameshikana yako hatarini iwapo hawataondolewa ukanda wa Gaza, kwa mujibu wa madaktari.

Alam Abu Hamna kutoka hspitali ya Shifa, ilisema kuwa hali inayowakumba watoto hao wasichana ni ngumu na kwamba haiwezi kutatuliwa na madaktari wa hospitali zilizo ukanda wa Gaza.

Ilisema kuwa matumaini ni kuwa watoto hao watasafirishwa ng’ambo ili watenganishwe

Watoto hao walizaliwa Jumamosi na mmoja wao anatajwa kuwa dhaifu kuliko mwingine.

Watoto hao walizaliwa Jumamosi na mmoja wao anatajwa kuwa dhaifu kuliko mwingine.

Hata hivyo kila mmoja ana moyo wake na mapavu. Mapacha ambao hutumia kiungo kimoja mara nyingi hukumbwa wna hatari ya kuishi.

“Maisha yao yako hatarini, ni hali iliyo ngumu,” Dr Abu Hamna alinukuliwa akisema na gazeti la Times la Israel.

Alisema hali ya mmoja wa mapacha hao iko shwari la mwenzake yuko hali mbaya na anahitaji matibabu.

“Ikiwa watasafirishwa nje kwa haraka kupata matibabu nje, maisha yao yataokolewa,” alisema.

Kitengo cha jeshi la Israel kinachohusika na kuratibu kuingia na kuondoka ukanda wa Gaza kinasema kuwa hakijapokea ombi lolote la mapacha kuondolewa eneo hilo.

Mapacha waliozaliwa wakiwa wameshikana katika Ukanda wa Gaza mwezi Novemba mwaka 2016 baadaye walikufa.

Israeli na Misri wameka vizuizi vya ardhini na baharinin kwa Ukanda wa Gaza kwa miaka kumi katika jitihada za kuzuia mashambulizi kutoka kwa wanamgambo.

Share this:

  • Click to share on Twitter (Opens in new window)
  • Click to share on Facebook (Opens in new window)
  • Click to share on Google+ (Opens in new window)

Related

Polisi Tanzania wawashikilia watu 12 kwa tuhuma za mapenzi ya jinsia moja
Ndoa za utotoni zakithiri Afrika Magharibi na Kati.

Related articles

Mabaki ya ndege iliotoweka na…
Refa Mkenya aliyeteuliwa na Fifa…
Rais Madagascar ateuwa waziri mkuu…
Bodi ya usimamizi wa shule…
Mchungaji auawa akiwabatiza waumini Ziwani
Volkano yasabisha vifo vya watu…

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

On Air Now

Download CG Google App here

CLICK TO PLAY CG ONLINE TV

Advertise here

ABOUT US

CG FM RADIO is the radio station that based in Tabora – Tanzania that targets all age groups. Due to its moral observation and ethical programs, CG FM radio continues to have a lot of audience which makes us the best on western zone.

YOU ARE HOME

TWITTER

My Tweets

Menu

  • HOME
  • News
  • Listen Live
  • Advertise