
Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira mjini…
Upatikanaji wa maji safi na salama katika kata ya MALOLO,Halmashauri ya Manispaa ya TABORA sasa imeimarika baada ya Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira mjini TABORA-TUWASA kufikisha huduma hiyo.
Diwani wa kata ya MALOLO,CORNEL NG’WANDU amesema kata hiyo ilikuwa haina huduma bora ya maji hali iliyowalazimu wananchi kutumia maji ya visima ambayo siyo safi na salama na kwamba TUWASA imesikia kilio chao na kutatua kero hiyo.
Amesema kwa visima ambavyo vilivyokuwa vimechimbwa, kwa sasa vimejengewa vizuri ili kuendelea kuyatunza maji hayo kwa ajili ya matumizi mengine.