
Matumizi ya fedha za kigeni hayasababishi kushuka kwa thamani…
Serikali imesema kuwa matumizi ya fedha za kigeni hayasababishi kushuka au kudorola kwa thamani ya fedha yoyote ile duniani.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango,ASHANTU KIJAZI amesema yapo mambo muhimu yanayosababisha misukosuko ya thamani ya fedha ya Taifa lolote ikiwemo mfumuko wa bei.
Naibu Waziri KIJAZI alikuwa akijibu swali la mbunge viti maalumu,DEVOTHA MINJA aliyetaka kujua ni lini serikali itapitia upya sheria zake na kuona uwezekano wa kulinda shilingi kama zilivyo nchi za KENYA na AFRIKA KUSINI.