Skip to content
CGFM
  • Home
  • Listen Live
  • News
  • Presenters
  • Gallery
  • Advertise

Miili 9 iliyokatwakatwa yapatikana kwenye nyumba Tokyo Japan.

  • October 31, 2017
Miili 9 iliyokatwakatwa yapatikana kwenye myumba Tokyo Japan.

Polisi nchini Japan wamemkamata mwanamume mmoja baada ya kupata viungo vya miili tisa katika nyumba yake iliyo Zama huko Tokyo.

Polisi walipata vichwa viwili kwenye jokovu nje ya nyumba ya mshukiwa kwa jina Takahiro shiraishi, wakati wakichunguza kutoweka kwa mwanamke mmoja.

Pia walipata viungo vya watu saba kwenye majokovu yaliyo ndani ya nyumba yake.

Mtu huyo wa umri wa miaka 27 anashtakiwa kuwa ndiye alitupa miili hiyo.

Polisi walikuwa wamepata miili ya wanawake 8 na mwanamume mmoja, mingine tayari ikiwa imeanza kuoza.

“Niliwaua na nikaifanyia kazi miili yao ili kuficha ushahidi,” shirika la habari la NHK lilimnukuu akisema.

Jirani wake alisema kuwa alikuwa ameanza kuhisi harufu mbaya kutoka kwa nyumba yake tangu Bw. Shiraishi ahamie nyumba hiyo mwezi Agosti.

Polisi walifanya ugunduzi huo walipokuwa wakimtafuta mwanamke wa umri wa miaka 23 ambaye amekuwa hajulikani aliko tangu tare 21 mwezi Oktoba.

Wachunguzi waligundua kuwa Bw. Shiraishi amekuwa akiwasiliana na mwanamke huyo baada ya kuandika kwenye mitandao ya kijamii kuwa alikuwa anataka kujiua.

Share this:

  • Click to share on Twitter (Opens in new window)
  • Click to share on Facebook (Opens in new window)
  • Click to share on Google+ (Opens in new window)

Related

Mtu aliyepanga kumuua Rais Vladimir Putin ajeruhiwa Ukrain.
Kiwango cha ukusanyaji wa damu katika Manispaa ya TABORA kimepungua kutoka chupa l,709 hadi chupa 828 kwa mwezi uliopita.

Related articles

Mabaki ya ndege iliotoweka na…
Refa Mkenya aliyeteuliwa na Fifa…
Rais Madagascar ateuwa waziri mkuu…
Bodi ya usimamizi wa shule…
Mchungaji auawa akiwabatiza waumini Ziwani
Volkano yasabisha vifo vya watu…

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

On Air Now

Download CG Google App here

CLICK TO PLAY CG ONLINE TV

Advertise here

ABOUT US

CG FM RADIO is the radio station that based in Tabora – Tanzania that targets all age groups. Due to its moral observation and ethical programs, CG FM radio continues to have a lot of audience which makes us the best on western zone.

YOU ARE HOME

TWITTER

My Tweets

Menu

  • HOME
  • News
  • Listen Live
  • Advertise