Skip to content
CGFM
  • Home
  • Listen Live
  • News
  • Presenters
  • Gallery
  • Advertise

Mike Pence aondoka uwanjani baada ya wachezaji kupinga ubaguzi

  • October 9, 2017
Makamu wa Rais wa Marekani Bw. Mike Pence.

Makamu wa rais wa Marekani Mike Pence, ameondoka kutoka kwa mechi ya kandanda ya NFL nchini Marekani, baada wachezaji kukataa kusimama wakati wa kuchezwa kwa wimbo wa taifa wa Marekani.

Bw. Mike Pence aliondoka uwanjani baada ya wachezaji wa San Francisco 49ers kugoma kusimama wakati wa kuimba wimbo wa taifa.

Bw. Pence alisema kuwa hatakuwa kwenye warsha ambayo haiheshimu wanajeshi wa Marekani au bendera baada ya kuondoka kwenye mechi iliyokuwa ikichezwa katika jimbo nyumbani kwake huko Indiana.

Aliondoka baada ya wachezaji wa timu ya San Francisco 49ers haikusimama wakati wa wimbo wa taifa kabla ya mechi dhidi ya Indianapolis Colts.

Rais Donald Trump aliandika katika mtandao wa twitter kuwa alimuomba Pence kuondoka ikiwa wachezaji wangepiga magoti.

Kupiga magoti wakati wa mechi za NFL imekuwa njia ya kupinga ubaguzi wa rangi.

Trump amewakosoa wachezaji vikali na kuitaka NFL kuwapiga marufuku.

“Niliondoka katika mechi ya leo kwa sababu rais Trump na mimi hatutakubali warsha yoyote ambayo haieshimu wanajeshi wetu, bendera yetu au wimbo wetu wa taifa,” Pence aliandika kwenye twitter siku ya Jumapili.

Wachezaji wa San Francisco 49ers hawakusimama jana wakati wa kuimba wimbo wa taifa wa nchi hiyo.

Aliondoka baada ya wachezaji wa timu ya San Francisco 49ers haikusimama wakati wa wimbo wa taifa kabla ya mechi dhidi ya Indianapolis Colts.

Awali Bw. Trump alisema kuwa matamshi yake ya kukosoa hatua za NFL hayakuhusu kwa vyoyote vile suala la rangi.

 

Share this:

  • Click to share on Twitter (Opens in new window)
  • Click to share on Facebook (Opens in new window)
  • Click to share on Google+ (Opens in new window)

Related

Kichwa cha mwandishi aliyetoweka chapatikana baharini Sweden
Uturuki na Marekani katika mzozo wa utoaji visa.

Related articles

Mabaki ya ndege iliotoweka na…
Refa Mkenya aliyeteuliwa na Fifa…
Rais Madagascar ateuwa waziri mkuu…
Bodi ya usimamizi wa shule…
Mchungaji auawa akiwabatiza waumini Ziwani
Volkano yasabisha vifo vya watu…

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

On Air Now

Download CG Google App here

CLICK TO PLAY CG ONLINE TV

Advertise here

ABOUT US

CG FM RADIO is the radio station that based in Tabora – Tanzania that targets all age groups. Due to its moral observation and ethical programs, CG FM radio continues to have a lot of audience which makes us the best on western zone.

YOU ARE HOME

TWITTER

My Tweets

Menu

  • HOME
  • News
  • Listen Live
  • Advertise