Skip to content
CGFM
  • Home
  • Listen Live
  • News
  • Presenters
  • Gallery
  • Advertise

Mkurugenzi Halmashauri ya Tunduru ang’olewa.

  • November 9, 2017November 9, 2017
Abdalla Mussa.

Dar es Salaam. Rais John Magufuli ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri (DED) ya Wilaya ya Tunduru, Abdallah Mussa kwa kushindwa kumudu majukumu yake.

Kutenguliwa kwa uteuzi wa mkurugenzi huyo leo Alhamisi Novemba 9,2017 kumefanyika siku tatu baada ya Rais Magufuli kutengua uteuzi wa wakurugenzi wengine wawili. Taarifa ya Rebecca Kwandu, mkuu wa kitengo cha mawasiliano serikalini katika ofisi ya Tamisemi imesema Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mussa Iyombe ndiye aliyotoa taarifa ya kutenguliwa kwa uteuzi huo leo mjini Dodoma. Amesema kutokana na hatua hiyo, uteuzi wa mkurugenzi mwingine utafanyika baadaye.

Rais Magufuli Novemba 6,2017 alitengua uteuzi wa wakurugenzi wa halmashauri za Manispaa ya Bukoba, Erasto Mfugale na wa Halmashauri ya Bukoba, Mwamtumu Dau. Viongozi hao walishindwa kutaja kiasi cha fedha za Mfuko wa Barabara zilizopokewa kwenye halmashauri zao walipoulizwa na Rais Magufuli wakati wa uzinduzi wa Uwanja wa Ndege wa Bukoba.

Alipoitwa mbele na kutakiwa kutaja kiasi halisi cha fedha zilizopokewa katika halmashauri kwa ajili ya mfuko huo, Mwantumu alijibu kuwa ana idara nyingi anazozisimamia hivyo isingekuwa rahisi kwake kukumbuka kila kitu, hivyo ni mpaka awepo mweka hazina. Pia, alisema hawezi kusema uongo.

Dk Magufuli katika mkutano huo alisema amewasamehe lakini baadaye Ikulu ilitoa taarifa ikieleza Rais ametengua uteuzi wao.

Share this:

  • Click to share on Twitter (Opens in new window)
  • Click to share on Facebook (Opens in new window)
  • Click to share on Google+ (Opens in new window)

Related

Trump na Xi waanza mazungumzo baada ya makaribisho ya kifahari
Hospitali ya Misheni Rulenge yaomba msaada kuokoa maisha ya majeruhi.

Related articles

Msanii Sam wa Ukweli ameaga…
Mazishi ya pacha Maria na…
Vladmir Putin aizuru Austria.
Jeshi la Zimamoto lakanusha madai…
TABORA: Biashara ya Magimbi yashamiri…
Serikali imetenga fedha kwa ajili…

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

On Air Now

Download CG Google App here

CLICK TO PLAY CG ONLINE TV

Advertise here

ABOUT US

CG FM RADIO is the radio station that based in Tabora – Tanzania that targets all age groups. Due to its moral observation and ethical programs, CG FM radio continues to have a lot of audience which makes us the best on western zone.

YOU ARE HOME

TWITTER

My Tweets

Menu

  • HOME
  • News
  • Listen Live
  • Advertise