Mwanasoka wa zamani GEORGE OPONG WEAH anaongoza katika matokeo…

Takwimu kutoka Tume ya Uchaguzi ya LIBERIA -NEC zinaonyesha kuwa WEAH yupo mbele kwa majimbo 11 katiKa ya majimbo 15 ingawa kura zote hazijahesabiwa.
Mgombea anayefuatia ni Makamu wa Rais JOSEPH BOAKAI,ambaye anaongoza katika jimbo moja na mengine yaliyobaki ameshika nafasi ya pili.
Mshindi katika kinyang’anyiro hicho analazimika kujipatia asilimi 50 ya kura zote ili aweze kutangazwa mshindi na kama hakuna mgombea atakayefikisha kiwango hicho,uchaguzi wa marudio unapaswa kufanyika mwezi ujao.
Atakayetangazwa mshindi anachukua nafasi ya mwanamke wa kwanza Afrika kuwa Rais Bi ELLEN JOHNSON SIRLEAF anayemaliza muda wake kwa mjibu wa katiba ya Liberia na ambaye pia ni mshindi tuzo ya Nobel.