MWANZA: Rais JOHN POMBE MAGUFULI amechangia shilingi miilioni tatu…
Rais JOHN POMBE MAGUFULI amechangia shilingi miilioni tatu kusaidia kuboresha shule mbili za sekondari za kata ya IGOGO jijini MWANZA.
Rais ametoa mchango huo kabla ya kufungua kiwanda cha VICTORIA MOULDERS kinachotengeneza bidhaa mbalimbali yakiwemo matanki na mifuko ya vifungashio.
Rais MAGUFULI pia ametoa shilingi milioni moja kwa uongozi wa Chama cha Mapinduzi-CCM kata ya IGOGO ili kuboresha matengenezo ya ofisi ya chama hicho.