
KENYA: Rais UHURU KENYATTA leo ameapishwa kuiongoza KENYA kwa…
Jaji Mkuu wa KENYA,DAVID MARAGA amemwapisha UHURU KENYATTA kuwa Rais katika sherehe kubwa iliyofanyika katika uwanja wa michezo wa MOI KASARANI mjini NAIROBI.
Sherehe za kuapishwa Rais UHURU zimehudhuriwa na viongozi wa mataifa mbali mbali akiwemo Makamu wa Rais wa TANZANIA,SAMIA SULUHU HASSAN aliyemwakilisha Rais Daktari JOHN POMBE MAGUFULI.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA na Waziri Mkuu wa zamani,EDWARD LOWASSA pia amehudhuhuria sherehe hizo.
Kabla ya kuapishwa kwa Rais KENYATTA,usalama uliimarishwa katika mji mkuu wa KENYA- NAIROBI.
Uchaguzi wa mwezi Agosti uliompa ushindi Rais KENYATTA ulifutwa na Mahakama ya Juu ya nchi hiyo kutokana na kile kilitajwa kuwa uchaguzi usio huru na haki.
Marudio ya uchaguzi wa Oktoba 26 ulimpatia UHURU KENYATTA ushindi asilimia 98 ya kura huku waliojitokeza kushiriki katika shughuli hiyo wakiwa asilimia 39.