Skip to content
CGFM
  • Home
  • Listen Live
  • News
  • Presenters
  • Gallery
  • Advertise

Ndoa za utotoni zakithiri Afrika Magharibi na Kati.

  • October 24, 2017

Licha ya kuwepo kwa upungufu wa kesi za ndoa za utotoni, nchi za Afrika Magharibi na Kati zimeshuhudia ongezeko la ndoa za utotoni.

Katika mkutano wa siku tatu ulionza Jumatatu huko nchini Senegal ulionuiwa kutokomeza ndoa za utotoni Afrika Magharibi na Kati, imebainika kwamba kwa wastani, binti mmoja anaezaliwa kati ya watatu katika eneo hilo ataolewa kabla ya miaka 18.

Idadi hiyo inafikia asilimia 76 nchini Niger.

Hali hii imeelezwa kuwa na athari kubwa katika elimu na afya ya wanawake na watoto, na vilevile kwa uchumi wa nchi, hii ni kwa mujibu wa Benki ya Dunia.

Siku ya kwanza ya mkutano huo, ambao ni wa kwanza kuwahi kufanyika nchini humo, washiriki wote wameonyesha kuwepo kwa dharura ya kutokomeza hali hiyo.

Mkutano huo unajumuisha mashirika ya kutoa misaada, mawaziri wa serikali mbalimbali, viongozi wa dini na wa jadi pamoja na viongozi kutoka mashirika ya Umoja wa Mataifa.

Waziri mkuu wa Senegal Mohamed Dione amesem kinachotakiwa sasa hivi ni kutoka katika nadhari na kuelekea katika vitendo.

Kwa mujibu wa Al Hadj Sheikh Abu Bakar Conteh, mjumbe kutoka Baraza la Dini nchini Sierra Leone, viongozi wa dini watakuwa sehemu muhimu katika kutatua tatizo hilo.

“Wana jukumu kubwa sana katika kuwalinda na kuwatetea wafuasi wao dhidi ya kila kitu chenye madhara, kama hili tunalozungumzia, ndio maana, kwa sisi hapa Sierra Leon, mpango wowote wa kijamii ili ufanikiwe, ushirikishwaji wa viongozi wa kidini ni lazima,” amesema Sheikh Abu Bakar Conteh.

Warsha na majadiliano yanaendelea mjini Dakar mpaka Jumatano.

Wanaharakati wanatumai kwamba mkutano huu utaleta mpango maalum na sheria, zitakazotokomeza ndoa za utotoni Afrika Magharibi na Kati kabla ya mwaka 2030.

Share this:

  • Click to share on Twitter (Opens in new window)
  • Click to share on Facebook (Opens in new window)
  • Click to share on Google+ (Opens in new window)

Related

Maisha ya pacha waliozaliwa wameshikana hatarini Gaza
Umoja wa Mataifa wataka wapinzani 30 kuachiwa huru DRC.

Related articles

Mabaki ya ndege iliotoweka na…
Msanii Sam wa Ukweli ameaga…
Refa Mkenya aliyeteuliwa na Fifa…
Mazishi ya pacha Maria na…
Rais Madagascar ateuwa waziri mkuu…
Bodi ya usimamizi wa shule…

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

On Air Now

Download CG Google App here

CLICK TO PLAY CG ONLINE TV

Advertise here

ABOUT US

CG FM RADIO is the radio station that based in Tabora – Tanzania that targets all age groups. Due to its moral observation and ethical programs, CG FM radio continues to have a lot of audience which makes us the best on western zone.

YOU ARE HOME

TWITTER

My Tweets

Menu

  • HOME
  • News
  • Listen Live
  • Advertise