
Ndovu wauaji wauawa kwa kupigwa risasi Msumbuji
Polisi wamewaua kwa kuwapiga risasi ndovu kwenye mkoa ulio kusini mwa Msumbiji wa Gaza, baada ya ndovu hao kumuua mwanamke mmoja na kumjeruhi mwingine.
“Polisi hawakuwa na lingine ila kuwaua ndovu hao kwa sababu walikuwa ni tatizo, na wangehatarisha maisha ya watu zaidi,” alisema mkurugenzi wa masuala ya mazingira Juliana Mwito.
Ndovu hao walikuwa wamevuka kutoka mbuga ya Afrika Kusini ya Kruger ambayo ni maarufu kwa watalii.
“Ndovu hao pia waliharibu mimea mingi na kuleta madhara kwa tegemeo a watu wanaoishi vijijini,” Bi Mwito alisema.