Nishati ya MAFUTA yapatikana katika bonde la mto MANONGA…

Tafiti za awali zinaonesha kuwa Bonde la mto MANONGA katika wilaya ya IGUNGA mkoani TABORA lina uwezekano wa kupatikana nishati ya mafuta.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini,Daktari Mhandisi JULIANA PALLANGYO amebainisha hayo kwenye mkutano wa hadhara katika kata ya KINUNGU wilayani IGUNGA.
Mhandisi JULIANA ametoa wito kwa wananchi wa eneo la bonde la mto MANONGA kushirikiana na watalamu mbalimbali watakaokwenda katika vijiji hivyo kufuatilia upatikanaji wa nishati ya mafuta katika eneo hilo.