Skip to content
CGFM
  • Home
  • Listen Live
  • News
  • Presenters
  • Gallery
  • Advertise

Obama na Bush wakosoa uongozi wa Trump.

  • October 20, 2017
Marais wawili wa zamani nchini Marekani George Bush (Kushoto) na Barrack Obama(Kulia).

Marais wawili wa zamani nchini Marekani wameonyesha wasiwasi wao kuhusu hali ya kisiasa nchini humo bila kumtaja rais Donald Trump kwa jina.

Barrack Obama aliwataka wapiga kura kukataa kile alichokitaja kuwa siasa za kuwagawanya watu mbali na siasa za hofu.

Alikuwa akimfanyia kampeni mgombea wa chama cha Democrat anayewania wadhfa wa gavana wa jimbo la New Jersey.

Matamshi yake yanajiri saa chache baada ya mtangulizi wake George W. Bush kukosoa unyanyasaji na chuki katika maisha ya kawaida ya raia Marekani.

Katika hotuba, alisema chuki dhidi ya wale wanaokupinga zimeongezwa nguvu huku maadili ya kiraia yakisahaulika.

Bwana Trump ambaye amekuwa mkosoaji mkubwa wa mtangulizi wake bado hajatoa tamko lolote.

Marais wa zamani nchini Marekani kwa kawaida huwa nadra kutoa maoni yao kuhusu hali ya kisiasa na ilionekana kuwa makosa makubwa kwa rais aliyetangulia kumkosoa mrithi wake katika ikulu ya Whitehouse.

lakini maadili na viwango vya tabia ambazo awali zilikuwa zikifuatwa sasa zimesahaulika katika mazingira ya kisiasa ya wakati huu.

Akizungumza katika mkutano wa kampeni za chama cha Democrat , mjini New Jersey, Obama alisema kuwa Wamarekani wanapaswa kutuma ujumbe kwa ulimwengu kwamba tunakataa siasa za kugawanywa na siasa za hofu.

Aliongezea: Kile ambacho hatufai kuendelea nacho ni kuwa na siasa za zamani za kugawanyana ambazo zimekuwepo nyakati za wali.

Siasa tunazoziona sasa tulidhani zimepitwa na wakati, hiyo ni kurudi miaka 50 nyuma.Ni karne ya 21 sio 19. jamani!.

Share this:

  • Click to share on Twitter (Opens in new window)
  • Click to share on Facebook (Opens in new window)
  • Click to share on Google+ (Opens in new window)

Related

Arsenal yapata ushindi wa tatu mfululizo Yuropa.
Odinga atafakari kuendelea na uchaguzi.

Related articles

Mabaki ya ndege iliotoweka na…
Refa Mkenya aliyeteuliwa na Fifa…
Rais Madagascar ateuwa waziri mkuu…
Bodi ya usimamizi wa shule…
Mchungaji auawa akiwabatiza waumini Ziwani
Volkano yasabisha vifo vya watu…

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

On Air Now

Download CG Google App here

CLICK TO PLAY CG ONLINE TV

Advertise here

ABOUT US

CG FM RADIO is the radio station that based in Tabora – Tanzania that targets all age groups. Due to its moral observation and ethical programs, CG FM radio continues to have a lot of audience which makes us the best on western zone.

YOU ARE HOME

TWITTER

My Tweets

Menu

  • HOME
  • News
  • Listen Live
  • Advertise