Skip to content
CGFM
  • Home
  • Listen Live
  • News
  • Presenters
  • Gallery
  • Advertise

Ofisa Mtendaji Mkuu wake, Brad Gordon na Ofi sa…

  • November 3, 2017November 3, 2017

KAMPUNI ya Acacia imebainisha kuwa Ofisa Mtendaji Mkuu wake, Brad Gordon na Ofi sa Mkuu wa Fedha, Andrew Wray wameachia ngazi katika nafasi hizo.

Acacia ni moja ya kampuni kubwa za uchimbaji wa madini ya dhahabu Afrika na ina migodi mitatu Kaskazini- Magharibi mwa Tanzania, ambayo ni Bulyanhulu mkoani Shinyanga, Buzwagi wilayani Kahama mkoani Shinyanga na North Mara wilayani Tarime mkoani Mara. Kampuni hiyo imetangaza kuwa wawili hao wataondoka rasmi Acacia mwishoni mwa mwaka huu.

Kuachia ngazi kwa viongozi hao wawili, kumekuja ikiwa ni takribani miezi miwili tangu kampuni hiyo ya Acacia kumaliza mgogoro wake na Serikali ya Tanzania kuhusu udanganyifu katika usafirishwaji wa makinikia ya dhahabu.

Mgogoro huo ulianza baada ya Rais John Magufuli kupiga marufuku kusafirishwa nje ya nchi kwa mchanga wa madini wa Kampuni ya Barrick kwa kile ambacho ilisema ni kuwepo kwa udanganyifu kuhusu thamani ya madini yaliyomo kwenye mchanga huo. Hata hivyo, viongozi haowawili waliojiuluzu pamoja na timu ya viongozi na watalaamu mbalimbali kutoka Tanzania wakiongozwa na Waziri wa Katiba na Sheria, Palamagamba Kabudi, walifikia makubaliano ya kumaliza mgogoro huo.

Makubaliano hayo ni pamoja na Barrick kuingia makubaliano na Serikali ya Tanzania ya kuilipa dola za Marekani milioni 300 (sawa na Sh bilioni 700) kama malipo ya kuonesha nia njema ya kufidia fedha zilizotokana na upotevu wa mapato kupitia biashara ya kampuni hiyo.

Hata hivyo, taarifa inayopatikana kwenye tovuti ya kampuni hiyo imeeleza kuwa, Peter Geleta ataiongoza kampuni hiyo katika kipindi cha mpito huku Jaco Maritz akiongoza kitengo cha fedha. Wateule hao wataanza kazi kuanzia Januari mosi, mwakani.

Akizungumzia kujiuzulu kwa Brad na Andrew, Mwenyekiti wa Acacia, Kelvin Dushnisky amenukuliwa na taarifa hiyo akisema, “Brad na Andrew wamekuwa kiungo muhimu katika uendeshaji na masuala ya fedha hapa Acacia kwa kipindi cha zaidi ya miaka minne. Kwa niaba ya bodi, ninapenda kuwashukuru kwa mchango wao kwenye kampuni. Tunawatakia kila la heri kwa siku za usoni.”

Share this:

  • Click to share on Twitter (Opens in new window)
  • Click to share on Facebook (Opens in new window)
  • Click to share on Google+ (Opens in new window)

Related

Speaker wa Bunge Job Ndugai Asema wabunge wapigwe msasa katika suala la maadili.
EU yatoa bilioni 130 kwa ajili ya usambazaji wa umeme vijijini.

Related articles

Msanii Sam wa Ukweli ameaga…
Mazishi ya pacha Maria na…
Vladmir Putin aizuru Austria.
Jeshi la Zimamoto lakanusha madai…
TABORA: Biashara ya Magimbi yashamiri…
Serikali imetenga fedha kwa ajili…

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

On Air Now

Download CG Google App here

CLICK TO PLAY CG ONLINE TV

Advertise here

ABOUT US

CG FM RADIO is the radio station that based in Tabora – Tanzania that targets all age groups. Due to its moral observation and ethical programs, CG FM radio continues to have a lot of audience which makes us the best on western zone.

YOU ARE HOME

TWITTER

My Tweets

Menu

  • HOME
  • News
  • Listen Live
  • Advertise