Skip to content
CGFM
  • Home
  • Listen Live
  • News
  • Presenters
  • Gallery
  • Advertise

Papa aizuru Myanmar inayotuhumiwa kwa mauaji ya waislamu wa…

  • November 27, 2017
Pope Francis.

Papa Francis anaanza ziara ya wiki nzima nchini Myanmar na Bangladesh leo Jumatatu, wakati wasiwasi unaendelea wa kimataifa kuhusu usalama na ulinzi kwa wasilamu wa Rohingya.

Anatarajiwa kukutana na Aung Sun Suu Kyi na mkuu wa jeshi Myanmar.

Hata kabla ya kuondoka Roma, Papa Francis alikuwa anakabailiwana kitendawili cha kidiplomasia: iwapo kuliita kundi dogo la waislamu Myanmar – Rohingya.

Ni jina lisilo tumika na serikali ya kiraia na jeshi – wakieleza kuwa ni wahamiaji haramu kutoka Bangladesh na kwahivyo hawapaswi kuorodheshwa kama mojawapo ya makabila nchini humo.

Kiongozi wa Myanmar akimpokea Pope Francis.

Lakini mashirika ya kutetea haki za binaadamu wanamuomba awaite hivyo, yakieleza kuwa nilazima Papa Francis aoneshe huruma kwa watu walionyimwa uraia na tangu Agosti wamekabiliwa na kile kamishna wa haki za binaadamu katika Umoja wa mataifa amekitaja kuwa ‘kinachoonekana kuwa mauaji ya kikabila’.

Zaidi ya WaRohingya 600,000 wamekimbilia mpakani – na wakimbizi wakielezea kukabiliwa na mauaji, ubakaji na kuteketezwa moto kwa vijiji – jeshi imekana tuhuma zote.

Papa atakutana na kiongozi wa Myanmarr – Aung Sun Suu Kyi – Jumanne – huenda ni jukumu zito kidiplomasia katika miaka yake minne kama kiongozi wa kanisa katoliki.

Chanzo: BBC

Share this:

  • Click to share on Twitter (Opens in new window)
  • Click to share on Facebook (Opens in new window)
  • Click to share on Google+ (Opens in new window)

Related

Auawa kwa kukatwa shingoni na mwenzake chanzo kikiwa ni ulevi uliopitiliza.
Hatari yaongezeka kwa mlima wa volkano kulipuka Bali.

Related articles

Mabaki ya ndege iliotoweka na…
Refa Mkenya aliyeteuliwa na Fifa…
Rais Madagascar ateuwa waziri mkuu…
Bodi ya usimamizi wa shule…
Mchungaji auawa akiwabatiza waumini Ziwani
Volkano yasabisha vifo vya watu…

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

On Air Now

Download CG Google App here

CLICK TO PLAY CG ONLINE TV

Advertise here

ABOUT US

CG FM RADIO is the radio station that based in Tabora – Tanzania that targets all age groups. Due to its moral observation and ethical programs, CG FM radio continues to have a lot of audience which makes us the best on western zone.

YOU ARE HOME

TWITTER

My Tweets

Menu

  • HOME
  • News
  • Listen Live
  • Advertise