Skip to content
CGFM
  • Home
  • Listen Live
  • News
  • Presenters
  • Gallery
  • Advertise

Picha za tembo waliochomwa moto yashinda tuzo

  • November 8, 2017
Picha za tembo wawili wanaoonekana wakiutoroka umati wa watu uliowachoma moto imeshinda tuzo kuu katika shindano la picha za wanyama pori.

Picha za tembo wawili wanaoonekana wakiutoroka umati wa watu uliowachoma moto imeshinda tuzo kuu katika shindano la picha za wanyama pori.

Picha ya Biplab Hazra inaonyesha tembo mtoto akichomeka moto huku yeye na tembo mkubwa wakitoroka kwa kuhofia maisha yao mashariki mwa India.

Akitangaza tuzo hiyo, jarida la Sancuary lilisema kwamba unyanyansaji wa aina hii unafanyika mara kwa mara.

Picha hiyo ilichukuliwa magharibi mwa Bengal ambako migogoro kati ya wanyama na binaadamu imekithiri.

Haijulikani ni nini haswa kilichotokea kwa wanyama hao katika picha hiyo ilioshinda tuzo ambayo ilipigwa katika wilaya ya Bankura.

Wilaya hiyo imekuwa ikigonga vichwa vya habari kwa vifo vya binadamu vinavyotokana na mzozo na tembo.

Ujumbe huo ulisema ”Umati wa wanaume waliokuwa wakiwazomea tembo hao ulikuwa ukiwachoma” wakati Biplab Hazra alipopiga picha hiyo.

Anakumbuka kelele za ndovu hao walipokuwa wakitoroka.

”Kwa wanyama hao wazuri ,wanaowavutia Jamii sasa wako katika hali ya mbaya”, aliongezea.

Picha hiyo imevutia wengi katika mitandao ya kijamii.

Mainak Mazumdar anayeishi Bankura, alisema kuwa wanakijiji ni wa kulaumiwa kwa kuharibu mazingira ya wanyama pori na kwamba tembo wamekuwa wakinyanyaswa ma kuteswa.

Lakini alisema tembo wamewatesa wanadamu kwa kuharibu mimea yao, mashamba na kuwaua wato wasio na hatia.

Share this:

  • Click to share on Twitter (Opens in new window)
  • Click to share on Facebook (Opens in new window)
  • Click to share on Google+ (Opens in new window)

Related

Syria yaitenga Marekani, makubaliano ya tabia nchi ya Paris.
TABORA: Ashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kumbaka mwanafunzi wa darasa la nne.

Related articles

Mabaki ya ndege iliotoweka na…
Msanii Sam wa Ukweli ameaga…
Refa Mkenya aliyeteuliwa na Fifa…
Mazishi ya pacha Maria na…
Rais Madagascar ateuwa waziri mkuu…
Bodi ya usimamizi wa shule…

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

On Air Now

Download CG Google App here

CLICK TO PLAY CG ONLINE TV

Advertise here

ABOUT US

CG FM RADIO is the radio station that based in Tabora – Tanzania that targets all age groups. Due to its moral observation and ethical programs, CG FM radio continues to have a lot of audience which makes us the best on western zone.

YOU ARE HOME

TWITTER

My Tweets

Menu

  • HOME
  • News
  • Listen Live
  • Advertise