Pochettino: Paulo Gazzaniga anajua.

Meneja wa klabu ya Tottenham Hotspur, Mauricio Pochettino amemmwagia sifa mlinda lango wa timu hiyo raia wa Argentina, Paulo Gazzaniga baada ya kuchomoza na ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Crystal Palace.
Spurs ikiwa nyumbani Uwanja wa Wembley ilichomoza na ushindi huo kupitia bao safi la mshambuliaji wa kimataifa wa Korea Kusini, Son Heung-Min dakika 64 ya mchezo na kupelekea matokeo kumalizika kwa ushindi huo.
Kufuatia kiwango bora kilichoonyeshwa na mlindalango wa Spurs, Paulo Gazzaniga katika harakati za kuokoa michomo kadhaa iliyokuwa ikilenga lango lake meneja wa kikosi hicho, Pochettino amesema nikiwango bora kabi kilichoonyeshwa na kipa wake.