
Rais JOHN POMBE MAGUFULI ameiagiza Jumuiya ya Wazazi nchini…
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi-CCM,Rais JOHN POMBE MAGUFULI ameiagiza Jumuiya ya Wazazi nchini kusimamia maadili ya Taifa ikiwa ni pamoja na wanawake wanaovaa nguo zinazoacha wazi sehemu zao za mwili.
Akifungua mkutano mkuu wa Tisa wa Jumuiya ya wazazi ya CCM mjini DODOMA,Rais MAGUFULI amesema Watanzania wamepoteza mwelekeo kwa kuvunja maadili na utamaduni wetu.
Rais MAGUFULI amevitaka vyombo vya habari,Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo pamoja na Mamlaka ya Mawasiliano TANZANIA-TCRA kuchukua hatua kudhibiti uvunjaji wa maadili ya Taifa.
Pia amepongeza mafanikio yaliyofikiwa na Jumuiya ya Wazazi ukiwemo umiliki wa shule mbali mbali na Chuo cha Sanaa cha KAOLE kilichopo BAGAMOYO mkoani PWANI.