
Rais MAGUFULI amewaagiza mabalozi wa TANZANIA kutafuta masoko ya…
Rais JOHN MAGUFULI amewataka mabalozi wanaoiwakilisha TANZANIA katika nchi mbalimbali duniani kuhakikisha wanatafuta masoko ya bidhaa za kilimo.
Rais MAGUFULI ametoa agizo hilo wakati wa uzinduzi wa programu ya kuendeleza sekta ya kilimo awamu ya pili katika ukumbi wa Mwalimu NYERERE jijini DAR ES SALAAM akisema uzalisahaji wa mazao utakapoongezeka ni lazima mabalozi wahakikishe TANZANIA inakuwa na soko la uhakika la kuuzia mazao ya bidhaa za kilimo.
Kwa upande wake,Mratibu wa Programu ya Kuendeleza sekta ya kilimo awamu ya pili,Mhandisi JANUARY KAYUMBE amesema lengo la utekelezaji wa programu hiyo kuleta mapinduzi katika sekta ya kilimo, kubadilisha mfumo wa kilimo wa uendeshaji wa shughuli za kilimo kuwa za kibiashara na baadaye kukuza uchumi wa nchi.
Akizungumza kwa niaba ya wakulima,wafugaji ,wavuvi na wafanyabiashara MAGEMBE MAKOYE amesema wako tayari kushirikiana na wataalamu na viongozi kuhakikisha wanafikia lengo lililokusudiwa na kuiomba serikali kuimarisha upatikanaji wa pembejeo za kilimo.
Naye Mwenyekiti wa Sekta Binafsi,Dakta REGINALD MENGI amesema sekta hiyo inaunga mkono programuu hiyo yenye lengo la kuleta mageuzi katika sekta ya kilimo na kupandisha kipato cha mkulima.
Rais MAGUFULI pia ameitaka Benki ya Kilimo TANZANIA kuacha kuwakopesha matajiri badala yake iwakopeshe wakulima wadogo wadogo kwa sababu benki hiyo imeanzishwa kwa ajili ya kuwasaidia wakulima.
MWANDISHI: STEPHANIA LAISON,CGFM