Skip to content
CGFM
  • Home
  • Listen Live
  • News
  • Presenters
  • Gallery
  • Advertise

Rais Magufuli avipa masharti Viwanda vya Sukari.

  • November 9, 2017November 9, 2017

RAIS John Magufuli amesema kama viwanda vya sukari nchini vitazalisha sukari ya kutosha ya kukidhi mahitaji ya soko la ndani, atapiga marufuku uagizaji wa sukari kutoka nje.

Rais aliyasema hayo jana mkoani Kagera alipotembelea kiwanda cha kuzalisha sukari cha Kagera. Alisema mahitaji ya sukari nchini ni tani 450, 000 lakini uwezo wa kuzalisha wa viwanda vyote kwa jumla ni tani 320,000 na hivyo kusababisha upungufu wa tani 130,000.

Kwa mujibu wa Rais, Kiwanda cha Sukari cha Mtibwa mkoani Morogoro kina uwezo wa kuzalisha tani 30,000, Kiwanda cha Sukari cha TPC mkoani Kilimanjaro tani 100,000, Kiwanda cha Sukari cha Kilombero mkoani Morogoro tani 109,000, Kiwanda cha Sukari mkoani Manyara tani 6,000, Kiwanda cha sukari cha Kagera tani 65,000 hadi tani 67,000 ingawa kwa mwakani kimepanga kuzalisha tani 75,000.

“Idadi ya watu Tanzania ni milioni 52, lakini idadi ya watu kwa Afrika Mashariki ni milioni 165 na Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za kusini mwa Afrika (SADC) ina jumla ya watu milioni 400, tunapoanzisha viwanda lazima tufikirie kwa upana, kwa viwanda vilivyopo, kila kiwanda kijiwekee malengo ya kuongeza tani za sukari ili tani zote 450,000 ziweze kupatikana mwaka huu, ili mnisaidie mimi kupiga marufuku sukari kutoka nje,” alieleza Rais Magufuli.

Alisema kuna viwanda vingine vinajengwa na mifuko ya hifadhi ya jamii kama vile NSSF ambavyo vitaongeza uzalishaji wa sukari nchini. Aidha, Rais aliwataka wananchi kuchangamkia fursa ya kujenga viwanda vya sukari kwa kadri ya uwezo walionao kwa kuwa soko la bidhaa hiyo ni kubwa.

Alisema Tanzania haiwezi kuchezewa kwa kufanywa kama dampo kwa sukari zilizokwisha muda wake wa matumizi kutoka nje. Alisema sukari za aina hiyo zina madhara makubwa kiafya kwa watu, ikiwemo kupata magonjwa mbalimbali kama vile saratani.

Alisema wafanyabiashara wasio waaminifu huleta nchini sukari zilizokwisha muda wake wa matumizi na kuzipakia kwenye mifuko ya sukari ya viwanda vya hapa nchini na kuwauzia wananchi.

Rais Magufuli aliupongeza uongozi na Bodi ya Kiwanda cha sukari cha Kagera kwa uwekezaji mkubwa wanaofanya tangu mwaka 2001. Alisema kiwanda hicho kiliathiriwa sana na Vita vya Kagera mwaka 1978-1979 kwa kuwa majeshi ya Idd Amin yalikipiga mabomu kiwanda hicho na kilianza kurudi taratibu mwaka 1982.

Kiwanda hicho kwa mujibu wa Rais kimeajiri watu 5,000, lakini pia kimesambaza ajira kwa watu wengine kama vile wasambazaji wa sukari na watengenezaji wa magunia. Alisema hao wote wamekuwepo kwa sababu ya kuwepo kwa kiwanda hicho.

Aidha, Rais Magufuli aliwapongeza vijana wasomi wa Kitanzania waliopata elimu kwenye vyuo vikuu vya hapa nchini namna wanavyoshiriki katika uzalishaji kiwandani hapo na teknolojia ya kisasa inayotumika kiwandani hapo.

Share this:

  • Click to share on Twitter (Opens in new window)
  • Click to share on Facebook (Opens in new window)
  • Click to share on Google+ (Opens in new window)

Related

Hospitali ya Misheni Rulenge yaomba msaada kuokoa maisha ya majeruhi.
TABORA: Serikali inaendelea na juhudi ya kuhakikisha tumbaku inanunuliwa.

Related articles

Msanii Sam wa Ukweli ameaga…
Mazishi ya pacha Maria na…
Vladmir Putin aizuru Austria.
Jeshi la Zimamoto lakanusha madai…
TABORA: Biashara ya Magimbi yashamiri…
Serikali imetenga fedha kwa ajili…

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

On Air Now

Download CG Google App here

CLICK TO PLAY CG ONLINE TV

Advertise here

ABOUT US

CG FM RADIO is the radio station that based in Tabora – Tanzania that targets all age groups. Due to its moral observation and ethical programs, CG FM radio continues to have a lot of audience which makes us the best on western zone.

YOU ARE HOME

TWITTER

My Tweets

Menu

  • HOME
  • News
  • Listen Live
  • Advertise