
RAIS MAGUFULI: Mfumo wa utoaji wa haki nchini bado…
Mwandishi: Najjat Omar
Rais JOHN POMBE MAGUFULI amesema usimamizi wa sheria na mfumo wa utoaji wa haki nchini bado unakabiliwa na matatizo mengi ikiwemo kupungua kwa maadili kwa watumishi wachache wenye dhamana ya kusimamia sheria.
Rais MAGUFULI ametoa kauli hiyo wakati wa akizungumza katika maadhimisho ya Wiki ya Sheria nchini akisema kuwa watumishi hao wachache hawapaswi kuachwa.
Rais MAGUFULI amesema hakuna mtu anayependwa kufukuzwa kazi,lakini Jaji Mkuu,Profesa IBRAHIM JUMA IBRAHIMa mefanya jambo jema kuwastaafisha watumishi hao.
Rais pia amevitaka vyombo ya usalama nchini kuiga mfano wa Jaji Mkuu kwa kuhakikisha wanatimia wajibu wao.
Kwa upande wake,Jaji mkuu wa TANZANIA,Profesa IBRAHIM JUMA amesema hataki kusikia kuwa jalada la kesi halionekani,limepotea wala kucheleweshwa kwa kesi.
Pia amewataka ,Majaji ,mahakimu na Watendaji wa mahakama kubadilika na kuendana na mabadiliko ya Teknolojia,Habari na Mawasiliano –TEHAMA kwa sababu mahakama zote nchini zitaungwanishwa katika mtandao wa TEHAMA.
Naye Makamu wa Rais wa Chama cha Mawakili TANGANYIKA,GODWIN GWIMILINI amesema kuwa lazima kuwepo na usawa wa mahitaji ya huduma na matakwa ya utawala.
Maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini mwaka yanaambatana na Kauli mbiu ya “Matumizi ya TEHAMA katika utoaji Haki kwa wakati na kuzingatia maadili.”