
Rihanna alizwa na Boxing Day
Inauma sana unapo ondokewa na mtu wako wa karibu. Rihanna amejikuta katika kipindi kigumu baada ya furaha ya kusherehekea sikukuu ya Christmas Jumanne hii kugeuka huzuni.
Msanii huyo amepatwa na msiba wa ndugu yake wa kiume [binamu yake] Tavon Kaiseen Alleyne, 29, ambaye amefariki dunia Jana baada ya kupigwa risasi katika maeneo ya St Michaels, Barbudos.
Tukio hilo limetokea baada ya kupita saa moja walipoachana ambapo Rihanna na Tavon walikuwa wakisherehekea pamoja sikukuu hiyo.
Riri ameonyesha kuumizwa sana na tukio hilo, kupitia mtandao wake wa Instagram ameandika ujumbe unaosomeka, “RIP cousin… can’t believe it was just last night that I held you in my arms! never thought that would be the last time I felt the warmth in your body!!! Love you always man! 😢🙏🏿❤ #endgunviolence.”