
Serikali imetenga fedha kwa ajili ya Mfuko wa Watu…
Serikali imetenga fedha kwa ajili ya Mfuko wa Watu wenye Ulemavu katika mwaka ujao wa fedha 2018-2019.
Kauli hiyo imetolewa bungeni jijini DODOMA na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu –Sera,Bunge,Ajira na Watu wenye ulemavu,STELLA IKUPA wakati akijibu swali la mbunge wa viti maalum AMINA MOLELI aliyetaka kujua ni lini serikali itatenga fedha kwa ajili ya mfuko wa watu wenye ulemavu.
Akiuliza maswali mawili ya nyongeza mbunge wa viti maalum AMINA MOLELI amehoji ni lini serikali itaunda Baraza la Watu wenye Ulemavu.
Akijibu maswali hayo,Naibu Waziri STELLA IKUPA amekiri kuwa muda wa wajumbe wa baraza la watu wenye walemavu kuongoza baraza hilo umekwisha.
Baraza la watu wenye ulemavu lilianzishwa kwa mujibu wa lengo la kuwezesha utekelezaji wa majukumu ya Baraza la Taifa la Ushauri kwa watu wenye ulemavu, hivyo serikali inajipanga kuhakikisha wanapatikana watu waaminifu na wenye uwezo wa kuwasilisha matatizo ya watu wenye ulemavu kwa muda muafaka.
MWANDISHI: ANGEL MTAKI,CGFM