Serikali ya KOREA KASKAZINI imeutaja mkataba wa kijeshi kati…

Gazeti la chama tawala nchini KOREA KASKAZINI limeandika kuwa, mkataba huo wa kijeshi ni njama ya wazi ya MAREKANI na mshirika wake KOREA KUSINI kwa ajili ya kufanikisha ndoto zao za kutaka kuishambulia ardhi ya nchi hiyo.
Gazeti hilo limeongeza kuwa,mkataba huo kati ya KOREA KUSINI na MAREKANIÂ ulifikiwa kupitia ujeuri na uhasama wa MAREKANI kwa ajili ya kuanzisha vita dhidi ya KOREA na kwamba unatakiwa uvunjwe mara moja kabla ya kupita wakati.

Limefafanua kuwa mkataba huo ndiyo msingi wa mazoezi ya kijeshi ya pamoja kati ya MAREKANI na KOREA KUSINI na kadhalika uwekaji wa vifaa vya kisasa vya kijeshi vya MAREKANI ndani ya ardhi ya KOREA KUSINI.
Kwa mujibu wa mkataba huo,kila nchi kati ya nchi hizo mbili inatakiwa kumsaidia kijeshi mwenzake wakati anaposhambuliwa na adui na ni kutokana na mkataba huo, ndipo MAREKANI ikatuma askari wake wengi nchini KOREA KUSINI.