
Serikali yatakiwa kuweka kukabiliana na ajali za barabarani.
Serikali imetakiwa kuweka mipango mikakati ili kukabiliana na ajali zinazotokana na uzembe wa madereva na kusababisha vifo visivyo vya lazima.
Kauli hiyo imetolewa bungeni jijini DODOMA na Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano ELIAS KWANDIKWA akisema tayari serikali imeishaanza kuchukua hatua ikiwa ni pamoja na kurekebisha barabara korofi.
Akiuliza swali la msingi,mbunge wa jimbo la VUNJO,JAMES MBATIA alitaka kujua ni lini serika itatatua tatizo la uzembe wa madereva wanaosababisha vifo vya watu wengi nchini.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano amewataka madereva wote nchini kuchukua tahadhari barabarani ili kuweza kuepukana na ajali zisizo za lazima.