SERIKALI yaweka mikakati kuwawezesha wahitimu wa ngazi za Elimu…
Serikali imesema imeweka mikakati mbalimbali itakayowawezesha vijana wahitimu wa ngazi mbalimbali za elimu kuweza kujiajiri wenyewe.
Akibu swali bungeni mjini DODOMA,Naibu Waziri wa Kazi,Ajira na Vijana,ANTONY MAVUNDE amesema baadhi ya mikakati inayotekelezwa mahsusi kwa ajili ya vijana ni mradi wa kukuza ujuzi nchini unaopatikana katika mfumo usio rasimi na kurasimisha kwa kutoa mafunzo ya muda mfupi.
Naye Mbunge wa viti maalumu AIDA KENANI ameuliza swali la nyongeza akitaka kujua kama serikali ya awamu ya tano imepunguza wafanyakazi katika kada mbalimbali kwa kigezo cha kutokuwa na sifa na lini serikali itatoa ajira kwa kuwapa kipaumbele vijana nchini ambao kwa sasa wapo mitaani kwa ukosefu wa ajira.