
STEPH CURRY aiongoza Golden State Warriors kushinda fainali dhid…
Mcheza mpira wa kikapu,STEPH CURRY wa timu ya GOLDEN STATE WARRIORS ya MAREKANI ameiongoza timu hiyo kushinda fainali ya pili ya ligi ya mpira wa kikapu nchini humo maarufu kama NBA baada ya timu yake kuwashinda CLEVELAND CAVALIERS vikapu 122 kwa 103.
CURRY amefunga alama thelathini na tatu huku alama 27 kati ya hizo akizipata kwa mabao tisa aliyofunga katika umbali mrefu.
Ushindi huo unakuwa wa pili kwa WARRIORS baada ya mchezo wa kwanza kushinda vikapu 111 wakiwafunga CAVALIERS vikapu 93 na kubakiza michezo miwili ya fainali msimu huu.