
TABORA: Biashara ya Baiskeli yadorora TABORA.
Biashara ya baiskeli katika Halmashauri ya Manispaa ya TABORA kwasasa imekuwa ngumu kutokana na kuadimika kwa wateja
Mfanyabiashara wa baiskeli RAMADHANI HERI,amesema kuwa utokaji wa baiskeli umekuwa mdogo tofauti na kipindi cha nyuma ambapo soko la baiskeli lilikuwa zuri.
Aidha amesema anakumbana na changamoto ya wateja kulalamika kupunguziwa bei wakidai wana hali ngumu ya kiuchumi
Kwa upande wao baadhi ya wateja wa baiskeli mjini TABORA Bwana JAMES STIVIN na MOHAMED BAKARI wamesema kuwa baiskeli zinawasaidia kurahisisha safari na kuwataka wafanyabiashara kupunguza bei ili wamudu kununua.