
TABORA: Jamii na wadau mbalimbali wahimizwa kuwaunga mkono watu…
Jamii na wadau mbalimbali mkoani TABORA wamehimizwa kuwaunga mkono watu wenye ulemavu kwa kuwapa nyenzo mbalimbali zitakazowawezesha kujiajiri wenyewe na kuondokana na tabia ya kuwa ombaomba.
Mmoja wa walemavu wa macho ambaye ni fundi seremala katika manispaa ya TABORA,HASSAN ATHUMAN amesema ameamua kufanya kazi hiyo kutokana na uzoefu lakini wakati umefika sasa kwa jamii na wadau kuwasaidia watu wenye ulemavu.
Amewataka watu wenye ulemavu kuacha kubweteka na badala yake waanzishe miradi mbalimbali kwa kujiajiri wenyewe kwa sababu serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Daktari JOHN POMBE MAGUFULI imeweka mazingira mazuri kwa watu wenye ulemavu.