
TABORA: Jamii yatakiwa kuwaelimisha wanawake ambao bado hawajaelimika kuhusu…
Jamii mkoani TABORA imetakiwa kuwaelimisha wanawake ambao bado hawajaelimika kuhusu haki zao. Mwalimu wa shule ya msingi ISIKE mjini TABORA,VAILETH KIRIGITO amesema katika kuelekea kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani inayofanyika Machi Nane kila mwaka,wanawake walioelimika wanatakiwa kuwaelimisha wenzao ambao hawajazitambua haki zao za msingi.
Naye Mwalimu LETICIA MZAGA amesema kila mwanamke atambue umuhimu wa kushiriki Siku ya Wanawake Duniani mkoani TABORA inayoratibiwa na CG FM yaani CG WOMEN GALA kwa sababu watapata fursa ya kukutana na wanawake na kujadiliana mambo mbalimbali yanayowahusu kijamii na kiuchumi.
Wote kwa pamoja wametoa wito kwa wanawake wa mkoa wa TABORA kujitokeza kwa wingi kushiriki kushiriki katika sherehe hizo zitakazofanyika katika viwanja vya CHIPUKIZI mjini TABORA kwa sababu ni fursa ya kipekee kwao ya kuonana na viongozi mbalimbali wa kitaifa na kujifungza mambo mengi mazuri yatakayowasaidia katika maisha yao.
Wamesema wanawake wote wa mkoa wa TABORA wanaojishughulisha na shughuli ndogondogo za kijasiriamali na wafanyakazi wa serikali wasiache kushiriki katika hafla hiyo maalumu inayowahusu wanawake.