
TABORA: Jeshi la Polisi lakabidhiwa vifaa vya mawasiliano na…
Jeshi la polisi mkoani TABORA limekabidhiwa vifaa vya kisasa vya mawasiliano vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 47 kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi-UNHCR kwa ajili ya kumairisha mtandano wake wa Teknolojia ya Mawasiliano-TEHEMA.
Akikabidhi vifaa hivyo,kwa Kamanda wa polisi mkoa wa TABORA, Mwakilishi wa UNHCR wilaya ya MPANDA,AGNES KANYONYI anataja vifaa hivyo vitakavyosaidia jeshi la polisi kuboresha mawasiliano kati ya wilaya ya KALIUA na polisi mkoa wa TABORA katika kukabiliana na uhalifu mkoani TABORA.
Akizungumza baada ya kupokea vifaa hivyo,Kamanda wa polisi mkoa wa TABORA,Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa polisi WILBROAD MUTAFUNGWA licha ya kulishukuru shirika la UNHCR kwa msaada huo amesema vifaa hivyo vimetolewa kwa muda muafaka kusaidia kupambana na vitendo vya uhalifu.
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi pia limelikabidhi jeshi la polisi nyumba za askari huko ULYANKULU zenye thamani ya shilingi milioni 174 na kituo cha polisi cha daraja C ULYANKULU,wilayani KALIUA kilichojengwa kwa gharama ya shilingi milioni 181.