TABORA: Kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Mwenyekiti wa WETCU…
Kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili aliyekuwa Mwenyekiti wa WETCU,GABRIEL MKANDALA na wenzake WATANO imetajwa mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa wilaya ya TABORA,EMMANUEL NGWIGANA .
Kesi hiyo imetajwa jana kwa ajili ya kusikilizwa,lakini haikusikilizwa kutokana na upepelezi kutokamilika.
Wakili wa serikali,TITO MWAKALINGA ameiambia mahakama hiyo kuwa upelelezi wa shauri hilo unaendelea na kwamba jalada la kesi hiyo tayari lipo kwa Mkurugenzi wa Mashtaka-DPP.
Mshitakiwa wa kwanza katika kesi hiyo,GABRIEL MKANDALA baada ya kusikiliza tamko la Jamhuri kuwa bado upelelezi unaendelea ameiambia mahakama kuwa angependa kuona upelelezi unafanyika haraka na kwa haki ili wajue kama wana kesi ya kujibu au la ili waachiwe huru kwa sababu ni zaidi ya miezi saba sasa wapo rumande bila kujua hatma yao.
MKANDALA na wenzake wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi tangu Machi mwaka huu na kesi hiyo imepangwa kutajwa tena katika mahakama ya wilaya ya TABORA tarehe 20 mwezi huu.