TABORA: Mkurugenzi Manispaa ya Tabora atakiwa kuyatatua matatizo ya…
Baraza la madiwani la halmashauri ya manispaa ya TABORA limemwagiza mkurugenzi wa Manispaa hiyo kutafuta ufumbuzi wa matatizo ya wananchi yanayowasilishwa na madiwani badala ya kuyaacha kama yalivyo.
Akitoa agizo hilo katika kikao cha kawaida cha baraza la madiwani kwa niaba ya madiwani wenzake,Diwani wa kata ya NDEVELWA,SELEMAN MAGANGA amesema wamekuwa wakieleza matatizo ya wananchi,lakini Mkurugenzi na watendaji wake hawayatafutii ufumbuzi matatizo hayo.
Naye Diwani wa kata ya TAMBUKARELI,ZINDUNA KISAMBA amemwomba Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini-TARURA kuwajengea mifereji ya kupitishia maji ya mvua katika kata ya TAMBUKARELI kwa sababu kipindi cha masika kimeanza na hivyo maji yanaweza kuingia katika makazi ya wananchi.