TABORA: SUPPHIRE CUP, Leo IKONOLA inacheza dhidi ya NSAGUZI…
Timu za soka za IKONOLA na NSAGUZI FC kutoka wilayani UYUI zinatarajia kukutana muda mfupi ujao katika fainali ya mashindano ya SUPPHIRE CUP mchezo utakaofanyika katika uwanja wa shule ya msingi ILALWANSIMBA.
NSAGUZI wamefikia hatua hiyo baada ya kuwatoa KIDATU FC katika mchezo wa nusu fainali wakati IKONOLA wao walitinga hatua hiyo baada ya kuwafunga wenyeji wa mashindano hayo ILALWASIMBA.
Mshindi wa mchezo huo ataondoka na kitita cha shilingi laki mbili na mchezo huo utatangazwa moja kwa moja na kituo hiki cha CG FM