
TABORA: TUWASA kuondoa miundombinu yake kwa waliovamia maeneo ya…
Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazigira Mjini TABORA-TUWASA imesema itaondoa miundombinu yake ya maji kwa wale waliovamia maeneo ya shule ya sekondari MILAMBO
Mwanasheria wa mamlaka hiyo bwana KITANGALALA LUGANO amesema kuwa watakuchua hatua hiyo kufuatia agizo la serikali la kuwataka wananchi waliovamia maeneo ya shule ya sekondari MILAMBO kuondoka mara moja.
Amewataka kulipa ankara ya maji mapema kabla ya kuondolewa kwa miundombinu ya maji ili kuepuka usumbufu wa kuchukuliwa hatua za kisheria kwa atakaye shindwa kulipa
Naye Afisa biashara wa TUWASA bwana BISWALO BENARD amesema hatua hiyo itasababisha kupoteza wateja wao kwani hawatajua mahali walipohamia ili wapelekewe huduma ya maji
Amewataka wateja hao kutoa taarifa ya sehemu watakazohamia ili wapelekewe huduma ya maji na kuwataka kuwa waaminifu kuhusu huduma za maji.