TABORA: Vikundi vya ulinzi shirikishi na polisi wasaidia kurejesha…
Doria zinazoendeshwa na jeshi la polisi na vikundi vya ulinzi shirikishi zimesaidia kupunguza vitendo vya uhalifu katika kata ya KIDONGO CHEKUNDU,Manispaa ya TABORA, hali iliyorejesha amani kwa wananchi.
Baadhi ya wakazi wa kata hiyo JOHN JOHN na ZENA ISMAIL wamesema kufuatia doria hizo kwa sasa wanaekeleza kazi zao za maendeleo kwa bidii na kwamba baadhi ya vijana wahalifu katika kata hiyo wamekamatwa.
Naye Diwani wa kata ya KIDONGO CHEKUNDU,IDD MSABAHA amesema kutokana na kuimarika kwa usalama katani hapo sasa eneo hilo ni salama kuishi tofauti na ilivyokuwa hapo awali.