TABORA: Wadau wa Elimu Manispaa ya TABORA watakiwa kushirikiana…
Wadau wa elimu katika halmashauri ya Manispaa ya TABORA wametakiwa kushirikiana kutatua tatizo la upungufu wa vyumba vya madarasa unaozikabili shule za msingi na kusababisha msongamano kwa wanafunzi.
Afisa Elimu Msingi Manispaaa ya TABORA,Mwalimu FUE THOMAS amesema shule za msingi zina upungufu wa vyumba vya madarasa 710 kati ya vyumba 1,322 vinavyohitajika.
Miongoni mwa shule zenye upungufu wa vyumba vya madarasa ni pamoja na shule za msingi za MAJENGO na MWINYI ambazo wanafunzi wake wanalazimika kusoma kwa awamu.