
TABORA: Waganga 86 wanaojihusisha na ramli chonganishi wakamatwa na…
Jeshi la polisi Mkoani TABORA limesema kuanzia januari mpaka novemba mwaka huu limefanikiwa kukamata waganga 86 ambao wanajihusisha na ramli chonganishi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa TABORA kamishna msaidizi mwandamizi wa polisi WILBROAD MUTAFUNGWA amesema hatua hiyo ya misako na kuwakamata waganga kumesadia kupungua kwa mauaji
Katika hatua nyingine kamanda MUTAFUNGWA amesema, jumla ya makosa dhidi ya maadili ya jamii 602 yameripotiwa kwa mwaka huu ikilinganishwa na makosa 373 yaliyoripotiwa mwaka jana.
Aidha jeshi la polisi Mkoani hapa katika kupambana na uhalifu limefanikiwa kukamata silaha aina ya SMG MBILI na kilo 28,973 za bangi.
Hata hivyo Kamanda MUTAFUNGWA amesema sababu zinazosababisha kuwepo kwa uhalifu katika baadhi ya maeneo ni wananchi kujichukulia sheria mkononi na tamaa za kimwili kwa matukio ya ubakaji.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa TABORA kamishna msaidizi mwandamizi wa polisi WILBROAD MUTAFUNGWA jeshi la polisi limejipanga kuendelea kuelimisha jamii kutojichukulia sheria mkononi
Pia kuimarisha misako na doria za magari pamoja na pikipiki kwenye barabara kuu za kuingia Mkoani TABORA.