
TABORA: Wakulima mkoani TABORA wameshauriwa kuacha kilimo cha mazoea.
Wakulima mkoani TABORA wameshauriwa kuacha kilimo cha mazoea na badala yake kuingia katika kilimo cha kisasa kwa kutumia pembejeo rafiki kwa mkulima.
Akizungumza na CG FM,Meneja Masoko wa kampuni ya YARA TANZANIA,LINDA LIYABA amesema katika msimu huu wa kilimo kampuni ya YARA imepunguza beiĀ ya mbolea za kupandia mazao kwa asilimia kumi ili kumrahisishia mkulima kupata mbolea hiyo.
Amewataka wakulima kwenda kwa Mawakala na kununua mbolea ya YARA kwa bei nafuu katika kipindi hiki cha msimu wa punguzo la bei.
Pia amesema mbolea za YARA ni bora zaidi katika kilimo cha kisasa na zinasaidia kuchochea mzizi wa mmea kustahimili upepo na mazao kutoharibika.