
TABORA: Wakulima wahimizwa kutunza miti ya mikorosho wanayopewa na…
Wakulima wilayani TABORA wamehimizwa kutunza miti ya korosho wanayopewa na Manispaa ili iwakwamue kiuchumi.
Mratibu wa zao la korosho ambaye ni Afisa Kilimo Manispaa ya TABORA, SAMSON KITUNDU amesema wakulima wamekitia vizuri kilimo cha zao la korosho kitakachowakomboa kiuchumi tofauti na zao la tumbaku linaloonekana kuwa na changamoto nyingi.
Wakulima ADAM SHUMBI wa kijiji cha IGOMBE,kata ya MISHA na PETER MSABAHA wa kijiji cha ITAGA,kata ya MISHA wameahidi kuachana na kilimo cha tumbaku na kujikita katika kilimo cha korosho