
TABORA: Wanachi watakiwa kuacha kutumia dawa kwa mazoea
Wakazi wa Manispaa ya Tabora kushauriwa kwenda vituo vya huduma za afya mara wanapougua badala ya kutumia dawa kwa mazoea. Wananchi wa Halmashauri ya Manispaa ya TABORA wameshauriwa kwenda kwenye vituo vya kutolea huduma za afya wanapougua ili kupata vipimo vya kitabibu badala ya kutumia dawa kwa mazoea.
Hayo yameelezwa na mganga mkuu wa zahanati ya MORAVIAN MILUMBANI Daktari LAMECK KISULILA amesema matumizi ya dawa bila utaratibu maalum ni chanzo cha magonjwa nyemelezi mwilini na hata kusababisha vifo.
Daktari KISULILA ameitaka jamii kuwa na desturi ya kupima afya pale wanapougua kwa sababu itasaidia kubaini aina ya ugonjwa na tiba inayohitajika na pia kupunguza madhara mengine mwilini yanayotokana na usugu wa dawa.
Nao baadhi ya wananchi wa mjini TABORA wamesema wanalazimika kutumia dawa bila kupima afya zao wanapougua kutokana na hali ngumu kiuchumi.
Ameishauri jamii kuepuka matumizi ya dawa bila mpangilio maalum hasa kwa watoto kwa sababu dawa zinapozoeleka mwilini zinasababisha wawe dhaifu.