TABORA: Wanafunzi wenye ulemavu wa macho na Ngozi katika…

Wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi -Albino na wenye ulemavu wa macho katika shule ya sekondari TABORA WASICHANA wamehimizwa kusoma kwa bidii ili kufikia malengo yao na kuisaidia jamii.
Mwenyekiti wa asasi isiyo ya kiserikali ya AFRICAN GOLDEN GIRLS ya DAR ES SALAAM inayojishughulisha na kusaidia vijana wa kike,ANNA JONALEMA ametoa rai hiyo wakati wa kuwakabidhi zawadi mbalimbali wanafunzi hao.
Amesema vijana hao wanahitaji hamasa ili kuongeza kasi ya kujifunza.
Mkuu wa kitengo cha elimu maalumu,Mwalimu STEVEN PIUS na Mwalimu AHMAD ISSA wameipongeza na kuishukuru asasi ya AFRICAN GOLDEN GIRLS kwa kuwatembelea na kuwapatia wanafunzi zawadi na kusema hali hiyo inaongeza ari na motisha ya wanafunzi hao kujifunza.