
TABORA: Wanakijiji wajiwekea sheria za kufanya Usafi.
Mwenyekiti wa mtaa wa MAKUNGU kata ya CHEMCHEM Manispaa ya TABORA KISUZI MSWANYAMA amesema wamejiwekea sheria ambazo zimesaidia kufukuliwa kwa mtaro wa barabara ya SIKONGE.
MSWANYAMA amesema anaendelea kuwahamaisha wananchi wa mtaa huo kuhakikisha kwamba kufikia Januari 16 mazingira yanakuwa safi.
HEMED KAMULIKA ni mkazi wa mtaa wa MAKUNGU mara nyingi hupenda kutumia muda wake kwa ajili ya kusafisha mazingira kama moja ya majukumu yake.
Naye JULIANA WILLFRED mwanamke mwenye familia anasema hupenda kusafisha mazingira kila anapoona yamechafuka
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtaa wa BARUTI kata ya CHEMCHEM FAUSTUS CHOMA amesema mtaa wake una mitaro mitatu lakini wanakabiliwa na changamoto kukosa mkondo wa maji licha ya kusafisha mitaro.
Ameongeza kuwa ili kukabiliana na changamoto hiyo wanaomba wapatiwe makaravati ili washirikiane na wananchi kuendelea kusafisha mitaro.
Barabara ya Madaraka ni barabara kuu inayopakana na mitaa mingi ya kata za Mwinyi na Chemchem IKIWEMO MAKUNGU,KALAMATA,BARUTI,KWIHARA na soko katika Manispaa ya TABORA.