
TABORA: Wananchi walalamikia zoezi la uandikishaji wa vitambulisho vya…
TABORA wamelalamikia zoezi la uandikishaji wa vitambulisho vya Taifa –NIDA kwamba wanatozwa fedha nyingi tofauti na mwongozo wa serikali.
Wakazi hao wamesema kuwa zoezi la uandikishaji vitambulisho vya Taifa limekuwa na mlolongo mrefu hadi kukamilisha usajili wa kitambulisho hali inayosababisha usumbufu kwao.
Msimamizi wa zoezi la usajili na utambuzi wa vitambulisho vya Taifa mkoa wa TABORA,EMILIANA TEMU amesema watu waliyokuwa wanajihusisha na utozaji wa fedha kwenye zoezi hilo ni tamaa zao lakini kiuhalisia zoezi la uandikishaji ni bure.
Mwenyekiti wa mtaa wa KAZEHILL katika Halmashauri ya Manispaa ya TABORA,JOHN MSUMENO amesema yeye alijiandaa vizuri kwenye upande wa vifaa ili kuepusha changamoto kwa wananchi wake na kwamba changamoto zilizotokea wilayani KALIUA pengine walikuwa hawajajipanga vizuri.
Naye HAROLD KILUNGU kutoka asasi inayojihusisha na masuala ya utambuzi, utawala bora na maendeleo mkoani TABORA-TACEDE amesema zoezi la uandikishaji wa vitambulisho halijahusisha elimu ya awali kwa wananchi kama ilivyo kwa zoezi la upigaji kura ambalo hufanyika vizuri.
Msimamizi wa zoezi la usajili na utambuzi wa vitambulisho vya Taifa mkoa wa TABORA EMILIANA TEMU ameiomba kamati ya ulinzi na usalama iwajibike ipasavyo kuimarisha ulinzi katika maeneo ya kujiandikishia ili zoezi lifanyike kwa amani na utulivu.