TABORA: Wananchi waonywa kutoendelea na ujenzi bila kufuata taratibu…
Wananchi katika Halmashauri ya Manispaa ya TABORA wameonywa kutoendelea na ujenzi bila kufuata taratibu na sheria za uendelezaji wa miji ili kuepuka kubomolewa nyumba zao.
Mhandisi wa Ujenzi wa Manispaa ya TABORA,MOHAMED ALMAS amesema kabla ya wananchi kuanza kujenga lazima kuwa na kibali cha ujenzi kisha kufuata maelekezo kutoka manispaa.
Mhandisi ALMASI ameongeza kuwa wananchi ambao wamejenga bila kufuata utaratibu na sheria kuhusu ujenzi wanatakiwa kwenda manispaa kupewa maelekezo na ambao wamejenga katika viwanja ambavyo siyo vya na maeneo ya wazi watabomolewa.