
TABORA: Wananchi washauriwa kudumisha lugha na tamaduni zao.
Watanzania wameshauriwa kudumisha na kuenzi lugha za asili na tamaduni muhimu za makabila yao ili zisipotee katika jamii.
Afisa Utamaduni Manispaa ya TABORA,MEDERICO KATUNZI amesema lugha za makabila ni ishara ya kumtambulisha mtu mkoa anakotoka na zinapaswa kudumishwa na kuenziwa.
FETY RAJAB na NAFTARI HAMAD ni wakazi wa mkoa wa TABORA wamesema lugha za makabila hazipaswi kusahaulika katika jamii ya mtanzania kwa sababu zinadumisha utamaduni wa walikozaliwa.
Kwa upande wao,OMARI SHABAN na HUSSEIN ABBAS ambao ni wenyeji wa mkoa wa KIGOMA wanaoishi mkoani TABORA wamesema wanaipenda asili ya lugha yao ya Kikabila na wanaizungumza kwa ujasiri bila kujali kuwa wapo mkoani mwingine.
Wamewataka wale wanaozikataa lugha za makabila yao hasa wanapokuwa mikoa mingine waache tabia hiyo kwa sababu watapoteza tamaduni na asili ya lugha ya makabila yao hasa kwa watoto wao