
TABORA: Wananchi washauriwa kutumia maji safi na salama ili…
Wananchi wa mkoa wa TABOLRA wameshauriwa kutumia maji safi na salama yaliyochemshwa,kuchunjwa na kuhifadhiwa kwenye chombo safi ili kuepukana na magonjwa ya matumbo.
Daktari wa wanawake kitengo cha afya ya uzazi na vizazi katika hospitali ya mkoa- KITETE,Daktari MNUBI BAGUMA amesema kuchemsha maji ya kunywa ni muhimu ili kuua bakteria wanaoishi kwenye maji na kusababisha homa ya matumbo, kuharisha na kutapika.
Daktari BAGUMA amesema wananchi wengi hasa wanaoishi vijijini hukosa maji safi na salama na kutumia maji kuyachemsha bila kujua madhara yake na wanapougua wanatumia gharama kubwa kujitibu.
Mmoja kati ya mwananchi anayeishi kijijini anayetumia maji ya visima,EMMANUEL ALI anasema analazimika kunywa maji machafu kutokana na uhaba wa maji katika eneo analoishi.
Kila mwaka TANZANIA huungana na nchi nyingine duniani kuhamasisha jamii kuchemsha maji ya kunywa ili kujikinga na magonjwa ya homa ya matumbo.